Wanawake wanapenda kufanya Tendo la ndoa kwenye mazingira haya – Utafiti.

Inaeleweka kuwa wapendanao iwe wanandoa au wapenzi hupenda kufanya mapenzi sehemu yenye mwanga hafifu au gizani.

Tofauti na watu na mataifa mengine, kwa Waafrika suala hilo ni siri na linahitaji faragha kukamilika. Lakini kwa baadhi ya watu imekuwa kero kutokana na kutamani kufanya tendo hilo gizani, huku wanawake wakitajwa kuwa vinara wa kuzima taa.

Utafiti mpya umebaini kuwa katika kila wanawake wanne, mmoja anapenda na anakuwa huru kufanya mapenzi gizani kwa sababu mbalimbali ikiwamo kutojiamini.
Carl Loudgers aliyeshiriki kwenye utafiti huo na kuwauliza wanawake zaidi ya 2,000 kwa kukusanya majibu kwa njia ya mtandao anasema walibaini asilimia 60 ya wanawake hao wanatamani kuwa na ujasiri wa kukutana kwenye mwanga lakini wanashindwa.

Anasema zaidi ya asilimia 75 walisema hawapendi miili yao, huku asilimia 66 wakisema wanaona aibu kutokana na mwonekano wao.

Utafiti huo uliofanywa na mtandao wa Weight Watchers, ulibaini asilimia 27 wanafanya mapenzi gizani kwa sababu hawaamini miili yao kama inavutia kwenye mapenzi.

Ulionyesha pia asilimia 38 ya wanawake na wanaume waliohojiwa walisema kuwa wanaamini wapenzi wao hawatawaona wanavutia wakiwa watupu.

Sheiilar Gregam miongoni mwa wanandoa waliohojiwa kwenye utafiti huo alisema jambo linalochangia hali hiyo ni mitandao. Alisema wanawake wanaoonekana wakiwa watupu kwenye mitandao ni wale wanaovutia kiasi ukijilinganisha nao inakuwa ngumu kukubali kukaa bila mavazi, huku wapo ambao wanavutia.

“Nikiangalia mastaa walivyo na maumbile ya kuvutia, baadhi yao wamezaa, natambua kuwa wapo wanaojirudishia wakiharibika kama mimi baada ya kuzaa, lakini nakosa kujiamini kabisa na ninaamini hao wanapendeza zaidi yangu,” alisema Sheiilar katika mahojiano ya utafiti huo.
Baadhi yao wamekuwa wakiona aibu ya vitu vilivyomo mwilini mwao kama matiti, alama za mwilini na makovu ya upasuaji.

Maziwa kuanguka baada ya kunyonyesha mara tatu.
Kuning’inia nyama za tumbo na kuongezeka uzito ni moja ya sababu za kuzima taa.
Matokeo ya utafiti huo pia umebaini wanawake wawili katika kila wanawake watatu huchukia kuangalia wanawake wenzao wakiwa hawajavaa nguo.

Ulibaini kuwa asilimia 60 ya wanawake hawapendi kabisa kujitizama wao wenyewe kwenye kioo wakati wa kuvua nguo.

Loveness Ayoub mkazi wa Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam anasema hupata wakati mgumu anapokutana na mwanaume mzuri kwa sababu hukosa kujiamini na hivyo hufurahia zaidi wakijamiiana gizani.

Anasema akijitizama na rafiki zake humwambia amenenepa, hivyo akiwa na mwanaume anayevutia huamini atamuacha kutokana na umbo lake lilivyo.

“Tangu nipo chuo rafiki zangu walikuwa wananishangaa nikivua nguo, kiasi kwamba sikuwa nafanya hivyo wakiwepo, hali hiyo imenijengea uwoga na kunipotezea kujiamini.

“Nikiwa na mwanaume mtu mzima huwa sijali kwa sababu naamini ameona wanawake wengi amekuja kwangu kwa ajili ya kupumzika na sihitaji kuwa naye maishani ukilinganisha na wanaovutia ambao natamani hata wanioe,” anasema Ayoub.

“Nimeoa nina watoto wawili na huyo mke wangu, lakini nikitaka kumuona vizuri umbo lake akiwa mtupu nimvizie anaumwa au kalala, tofauti na hapo hajawahi kuvua nguo akakaa mbele yangu,” anasema Omari Kiyungi.

Kiyungi anasema licha ya kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka tisa mkewe hataki kabisa kukaa mtupu mbele yake kwa madai ya kuona aibu.

“Sipendi, natamani nimuone akiwa hajajiziba na ‘manguo’, lakini juhudi zangu zimegonga mwamba, hana dalili hiyo na hataki kabisa,” anasema.

Anasema alikuwa anachukia hadi sasa amezoea na akimuona mwanamke amevaa kihasara hasara anamdharau na kumuona hajiheshimu kwa sababu amezoea kufichiwa maungo.

Alisema akitizama mwili wake kwenye kioo hasa baada ya kuzaa mara mbili na kunenepa huogopa na kuhisi anamuangusha mumewe kwa umbile lake.

Msimamizi mkuu wa utafiti huo na mshauri wa masuala ya saikolojia Keren Smedley alisema wengi wa waliobainika kuona aibu kuvua nguo mbele ya wapenzi wao hawakuwa na tatizo na walikuwa na kila sifa ya kumshawishi mtu kuwatizama.

Akizungumzia hali hiyo mfundaji kutoka Mbagala Charambe, Zakia Kilimi maarufu Mchambaji, anasema wanawake wamekuwa na hali hiyo kutokana na tamaduni za siku za nyuma kuwa mapenzi hufanywa kwa siri.

Anasema wakati huo hasa kwa familia za kawaida walikuwa wanaishi katika chumba kimoja, hivyo upende usipende utazungumza na mwenzi wako gizani.

“Hii hali imesababisha hata wanawake wengi kushindwai kuachia hisia zao kwa wapenzi wao wakiamini wataonekana malaya na wasio na maadili kwa sababu imezoeleka mambo hayo ni ya kunyata nyata,” anafafanua.

Anaongeza kuwa siku hizi hayo mambo ndiyo yanakwisha na wanawake bila kujali wana umbo zuri, baya, makovu wanajiachia na kutambua umuhimu wa faragha ni kuonana hivyo wazazi wasiwatishe watoto wa kike kuwa kujiachia ni uhuni.

Zainabu Jumanne (siyo jina lake halisi) anasema kuwa mpenzi wake anajivunia kuwa naye lakini wakiwa faragha anashindwa kukaa mtupu. Anasema vivyo hivyo hata wanapojamiiana kukiwa giza hufanya kila aina ya mbwembwe tofauti taa ikiwa inawaka.

Anafafanua kwa sababu hiyo mumewe akitaka kuburudika na kukata kiu ya kuzungumza naye faragha huzima taa kabla hajaambiwa.

“Sijiamini kabisa kukiwa na taa, nahisi kama ananichora ninavyoweweseka, lakini kukiwa giza ashindwe yeye tu,” anasema.

Anaitaja sababu nyingine ya kupenda kujamiiana gizani ni matiti yake yamelala halafu hayana nyama.

Anasema anatumia ufundi wa faragha kuziba yote hayo kwa kumuonyesha mitindo mipya, lakini ili ayapate hayo sharti iwe gizani.

“Kukiwa giza akakubali kukutana nami, akiniacha nitatambika sina historia ya kuachwa tangu nikiwa msichana hadi nimeolewa, ingekuwa najiamini na kujamiiana kwenye mwanga na mautundu niliyonayo, naamini ningekuwa mkali zaidi, nimejaribu nimeshindwa na kwa hapa nilipofika haiwezekani tena,” anasema.

Mkazi wa Tandika jijini Dar es Salaam, Yusufali Yusuph anasema hataki hata kumsogelea mwanamke anayependa kujamiiana gizani kwa sababu huamini kuna kitu anaficha.
Anasema siku hizi maradhi mengi, anaweza kudhani anaona aibu au hajazoea kumbe kuna jambo anaficha.

“Haa raha ya mapenzi muonane jamani gizani tena! Siwezi na simtaki mwanamke wa aina hiyo,” anasema Yusuph.

Mtaalamu wa masuala ya saikolojia Modester Kamongi anasema yapo mambo mengi yanayochangia mwanamke kuogopa ikiwamo kutokujiamini.

Anasema mila, desturi na tamaduni ni miongoni mwa mambo yanayochochea hilo kwa sababu wanawake wengi huamini stara ndiyo sifa ya kuwa mke bora na kushindwa kutofautisha mahali pa kujistiri pa kujiachia.

Kamongi anasema linapokuja suala la aibu siyo kwa wanawake pekee wapo wanaume wenye aibu na wameumbwa hivyo, ikitokea kukutana na mmoja wa watu hao cha kufanya ni kuwazowesha taratibu hatimaye kama binadamu watakubaliana na hali halisi japo kwa shida.

“Huwachukua muda kuzoea, lakini uwezekanao upo na wakasahau kabisa kama walikuwa hawawezi, lakini inahitaji utayari wa kuwazowesha badala ya kuwalazimisha, ”alisema Kamongi.

Anaitaja sababu nyingine inayochangia wanawake kukataa kukaa utupu kuwa ni kutojiamini.
Anasema hali hii hutokana na maneno anayosikia au aliyosoma kuhusu umbo lake.

Anafafanua kuwa kuna baadhi ya familia mtoto akiwa mnene au mwembamba au ana umbo fulani uhusisha umbo hilo na neno ukiolewa sijui itakuwaje.

“Mtoto hukuwa na neno au misemo ya aina hiyo hivyo anapoolewa au kuwa na mpenzi hukumbuka na kutamani asimuone kwa sababu hajui itakuwaje kama alivyokuwa anaambiwa.

“Wengine hudhani mwanaume akiona umbile lake ambalo lilikuwa linawaisha ndugu, rafiki zake litamtisha pia na kuamua kumuacha, hivyo huona afadhali nusu shari kuliko shari kamili ya kuachwa,” anasema Kamongi.

Anaeleza wote hao wanaweza kubadilika iwapo wataeleweshwa na kujengewa kujiamini ikiwamo kwa kusifiwa kila wanapokaa bila nguo hata kwa bahati mbaya.

“Wengi wao hawajiamini, wakisifiwa na muhusika kuonyesha kutamani kuona maumbile yao mazuri yakiwa wazi taratibu watabadilika,” anasema.

Ushauri wazazi wawajenge watoto wa kike kuthamini vile alivyo navyo hususan kuukubali mwili wake badala ya kuwasema kwa ubaya kwa eneo lolote la mwili lililozidi au kupungua.